1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA: Mjumbe wa Umoja wa Ulaya ziarani Kongo

28 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDHU

Mjumbe maalum wa Umoja wa Ulaya katika kanda ya maziwa makuu barani Afrika,bwana Aldo Ajello yupo Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kwa ziara ya juma moja.Wakati wa ziara hiyo anakutana na Rais Joseph Kabila na makamu wa rais Jean-Pierre Bemba ambao watakumbana tena katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais tarehe 29 mwezi wa Oktoba. Mapambano kati ya wanajeshi walio tiifu kwa Kabila na Bemba yalisababisha vifo 23 mjini Kinshasa,lakini hali ya utulivu imerejea tangu jumanne iliyopita,baada ya pande hizo mbili kuviamuru vikosi vyao kuondoka barabarani.