1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA : Mchakato wa kusalimisha silaha wachapuka

29 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFSa

Kusalimisha silaha kunakofanywa na wanamgambo katika jimbo la kaskazini mashariki la Ituri katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kumepamba moto kufuatia kuwekwa tarehe ya mwisho ya kusalimisha silaha hizo hapo Ijumaa na Umoja wa Mataifa.

Kanali Laurent Banal mratibu wa kusalimisha silaha wa Tume ya Taifa ya Kuvunjwa kwa Makundi ya Wanamgambo na Kujumuishwa katika Jamii amesema kumekuwepo na ushahidi wa kuchapuka kwa mchakato huo wa kusalimisha silaha.

Banal amesema zaidi ya watu 2,000 wamekabidhi silaha zao katika siku za hivi karibuni huko Aru kaskazini ya Ituri.

Katika eneo jengine huko Bunia kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataiifa nchini Congo MONUC pia kimeshuhudia kuongezeka kwa usalamishaji silaha ambapo katika kipindi cha wiki mbili zilizopita jumla ya wanamgambo 6,000 huko Ituri imeripotiwa kuwa wamesalimisha silaha zao.