1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kimbunga Ida chapungua kasi Marekani

30 Agosti 2021

Kimbunga Ida kimewasili kwenye jimbo la Louisiana la kusini mwa Marekani lakini kimepungua kasi. Kituo cha kitaifa cha hali ya hewa kimesema kimbunga hicho sasa kimekuwa dhoruba ya kawaida ya kipindi cha joto.

https://p.dw.com/p/3zgTa
USA Hurrikan Ida | Gulfport
Picha: Steve Helber/AP/picture alliance

Kasi yake imepungua na kufikia kilometa 95 kwa saa. Hata hivyo bado pana hatari ya kutokea mafuriko, upepo mkali na maporomoko kwenye sehemu za kusini mashariki ya jimbo la Louisiana.

Jimbo hilo lilikumbwa na kimbunga kikali cha Ida kilichofikia mwendo wa kilometa 240 kwa saa hapo jana. Kiwango cha madhara bado hakijajulikana kwa uhakika hata hivyo mtu mmoja amekufa.