1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAsia

Kimbunga Doksuri chawahamisha maelfu China

31 Julai 2023

Mamia kwa maelfu ya watu wamehamishiwa kwenye mji mkuu wa China, Beijing, kukwepa kishindo cha kimbunga kikali kilichopewa jina la Doksuri ambacho kimeambatana na mvua kubwa iliyosomba magari na nyumba.

https://p.dw.com/p/4UapN
Unwetter in China I Doksuri
Picha: Lisa Marie David/REUTERS

Kimbunga hicho kilichookuwa kikielekea kaskazini mwa China, tayari kilishasababisha maafa kwenye jimbo la kusini la Fujian mwishoni mwa juma kilipowasili kutokea Ufilipino. 

Mbali ya Beijing, Kimbunga Doksuri kilisababisha mvua ya kiwango kilivyovunja rikodi kwenye mji wa Tianjin na mkoa jirani wa Habei. 

Wataalamu nchini China walionya kuwa kiwango hicho cha mvua huenda kingelisababisha mafuriko makubwa kushinda yale ya mnamo Julai mwaka 2012 ambayo yaliwaua watu 79 na kuwalazimisha mamia kwa maelfu ya wengine kuhamishwa.