1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kimbunga Beryl chaipiga Jamaika

4 Julai 2024

Kimbunga Beryl kimeipiga Jamaika jioni ya jana, kiking'owa miti, kuezuwa mapaa na kuharibu mashamba huku visiwa kadhaa cha Karibiki vikikabiliwa na pepo kali na mafuriko makubwa kwa siku kadhaa sasa.

https://p.dw.com/p/4hqJ9
Kimbunga Beryl
Kimbunga Beryl kikishambuilia visiwa vya Karibiki.Picha: AP Photo/picture alliance

Idadi ya awali ya waliopoteza maisha kwenye kimbunga hicho imefikia watu tisa, lakini inahofiwa kuwa ya juu zaidi.

Waziri Mkuu wa Jamaika, Andrew Holness, amewaambia waandishi wa habari kuwa raia wapatao 500 wamehifadhiwa kwenye maeneo mbalimbali. Viwanja vya ndege vimefungwa nchini humo kutokana na kimbunga hicho.

Athari kubwa zaidi za kimbunga hicho zimeshuhudiwa kwenye visiwa vya St. Vicent na Grenadine, ambako Waziri Mkuu Ralph Gonzales, amesema kuwa kisiwa cha Union kimeghariki kabisa. Zaidi ya asilimia 90 za nyumba kwenye kisiwa hicho kidogo zimeharibiwa.