1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Kim Jong Un atembelea viwanda vya uzalishaji silaha

10 Januari 2024

Shirika la habari la serikali ya Korea Kaskazini KCNA limeripoti siku ya Jumatano kuwa Kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un alitembelea wiki hii viwanda vya uzalishaji silaha.

https://p.dw.com/p/4b2pX
Kiongozi wa Korea Kaskazini  Kim Jong Un akiwa na binti yake
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un (kulia) akiwa na binti yake Kim Ju Ae wakati walipotembelea kiwanda cha uzalishaji silaha Januari 5,2024Picha: KCNA via REUTERS

Katika ziara hiyo, Kim alikosoa kile alichokiita "mapungufu" katika mfumo wa utengenezaji wa baadhi ya silaha huku akitoa wito wa kufanyika marekebisho na kusisitiza "umuhimu wa kimkakati wa uzalishaji wa silaha kubwa."

Soma pia:Korea Kaskazini yafanya luteka za kijeshi mpakani na Korea Kusini

Kim Jong Un amegusia pia mahusiano mabaya na jirani yake Korea Kusini na kuishutumu Seoul kuchochea mapigano huku akihimiza nchi yake kuimarisha nguvu zake za kijeshi pamoja na kuzidisha uwezo wa kujilinda wa silaha zake za nyuklia.