1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Kim Jong Un asifu mafanikio ya Korea Kaskazini mwaka 2023

27 Desemba 2023

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Yong Un, amesema mwaka 2023 umekuwa wa mabadiliko makubwa kwenye taifa hilo, akisifu mafanikio yaliyopatikana ndani ya jeshi na sekta nyingine ikiwemo uchumi, sayansi na afya ya umma.

https://p.dw.com/p/4abEz
Kiongozi wa Korea Kaskazini,Kim Yong Un
Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Yong Un.Picha: KCNA/REUTERS

Hayo yameripotiwa na shirika la habari la Korea Kaskazini, KNCA,  likinukuu matamshi ya Kim wakati wa hotuba yake ya kuufungua mkutano wa kila mwaka wa Kamati Kuu ya chama tawala cha kikomunisti cha nchi hiyo.

Kwa mujibu wa KNCA, Kim amewasilisha mbele ya wajumbe ripoti pana ya tathmini ya uchumi wa taifa ambao amesema unastawi vizuri chini ya misingi ya kikomunisti.

Mkutano huo unafanyika siku chache kabla ya kumalizika mwaka 2023 ambao umeshuhudia Korea Kaskazini ikijitangaza rasmi ndani ya katiba yake kuwa dola yenye uwezo wa nyuklia na kufanikiwa kurusha satelaiti ya kwanza ya kijeshi miezi michache iliyopita.