1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Kim Jong Un amaliza ziara Urusi, azawadiwa droni

17 Septemba 2023

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amehitimisha ziara yake nchini Urusi, na amerejea nyumbani akitokea eneo la mashariki la taifa hilo akitumia treni yake ya kijeshi.

https://p.dw.com/p/4WRSy
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un akiwaaga maafisa wa Urusi wakati akiondoka baada ya kuhitimisha ziara yake nchini Urusi, Septemba 17, 2023
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un akiwaaga maafisa wa Urusi wakati akiondoka baada ya kuhitimisha ziara yake nchini Urusi, Septemba 17, 2023Picha: Yuri Smityuk/TASS/picture alliance

Shirika la habari la Urusi, Ria Novosti limechapisha video iliyoonyesha hafla ya kuondoka kiongozi hiyo wa Korea Kaskazini Kim Jong Un katika kituo cha Artyom-Primorsky-1.

Shirika jingine la habari la Urusi TASS limesema  treni hiyo ya kijeshi inasafiri kwa mwendo wa takriban kilomita 250 kwa saa kuelekea mpakani.

Kulingana na TASS, kiongozi huyo alipewa droni tano za vilipuzi na nyingine tano za uchuguzi pamoja na fulana ya kuzuia risasi kama zawadi kutoka kwa gavana wa eneo hilo.

Ziara hii ya Kim imechochea hofu kwa mataifa ya Magharibi kwamba Moscow na Pyongyang huenda zitakaidi vikwazo na kufikia makubaliano ya silaha.