1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Kim Jong Un akutana na ujumbe wa China

27 Julai 2023

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, amekutana na ujumbe wa China ulioongozwa na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti, Politburo.

https://p.dw.com/p/4USIP
Nordkorea | Li Hongzhong und Kim Jong Un
Picha: KCNA/REUTERS

Shirika la habari la Korea Kaskazini limeeleza kuwa Kim leo amemkaribisha Li Haongzhong mjini Pyongyang, ambapo alimkabidhi barua rasmi ya Rais wa China, Xi Jinping.

Kim amekutana pia Waziri wa Ulinzi wa Urusi, Sergei Shoigu, ambapo walikuwa na mazungumzo ya kirafiki.

Soma zaidi: Korea Kaskazini yarusha makombora mawili, baada ya nyambizi ya Marekani kuwasili Korea Kusini

Shoigu alimkabidhi pia Kim barua iliyoandikwa na Rais wa Urusi, Vladmir Putin.

Urusi, mshirika wa kihistoria wa Korea Kaskazini, ni mojawapo ya mataifa machache ambayo Pyongyang imedumisha uhusiano wa kirafiki.

Korea Kaskazini leo inaadhimisha miaka 70 ya makubaliano ya kusitisha mapigano ya mwaka 1953, ambayo yalimaliza uhasama kati ya Korea Kaskazini na Korea Kusini.