1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kim Jong Un ajitokeza baada ya minong'ono kuhusu afya yake

Sekione Kitojo
2 Mei 2020

Kufuatia mbio ambazo ni za kiuchokozi katika majaribio ya makombora na silaha za nyuklia mwaka 2017,Kim alitumia michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi Korea kusini kuanzisha majadiliano na Marekani na Seoul mwaka 2018.

https://p.dw.com/p/3bfum
Nordkorea veröffentlicht neue Bilder von Kim Jong-Un
Picha: picturealliance/AP Photo/KCNA

Hatua  hiyo  ilisababisha  wimbi  la  mikutano, ikiwa  ni  pamoja  na mitatu  kati ya  Kim na  Trump.

Lakini  majadiliano  hayo  yameshindwa  katika  miezi  iliyopita kutokana  na  kutokubaliana katika  kubadilishana  na  unafuu  wa vikwazo  pamoja  na  hatua za  kuachana  na  utengenezaji  wa silaha, ambao  ulizusha  shaka  juu  ya  iwapo  Kim kama ataondoa kabisa  hazina  yake  ya  silaha ambayo  anaiona  kuwa  ni nguzo yake  imara  ya  kuendelea  na  shughuli  zake.

Nordkorea | Machthaber Kim Jong Un
Kim Jong Un katika mkutano wa wa chama tawala mjini Pyongyang Aprili 11, 2020 Picha: picture-alliance/AP Photo/Korea News

Kim aliingia  katika  mwaka  2020  akiapa  kujenga  hazina yake  ya silaha  za  nyuklia na  kuvishinda  vikwazo  kwa  kutumia "uchumi  wa kujitegemea."

Baadhi  ya  wataalamu  wanasema hatua ya  Korea ya kaskazini  ya kuwazuwia  watu  kutoka  nje  katika  wakati wa  mzozo wa  virusi vya  corona kunaweza  kuzuwia  kwa  kiasi  kikubwa  uwezo wake wa  kuwahimiza  watu  kufanyakazi.

Shirika  la  habari la  KCNA limesema  wafanyakazi  katika  kiwanda cha  mbolea  walianza ," kushangiria kwa  nguvu" wakimshangilia Kim, ambao shirika  hilo  lilisema , analiongoza  taifa  hilo  katika mapambano ya  ujenzi  wa  uchumi  wa  kujitegemea kutokana na "upepo mkali unaokuja"  kutoka  kwa  "nguvu hasimu."

Ripoti  hiyo  haikueleza  maelezo  ya  moja  kwa  moja  kuelekea Washington  ama  Seoul.

Nordkorea veröffentlicht neue Bilder von Kim Jong-Un
Mara baada ya kuzindua kiwanda cha mbolea tarehe 02.05.2020 KimJong Un anazungumza na viongozi wengine wa nchi hiyoPicha: picture-alliance/dpa/KCNA

Marekani  haikutajwa

Akizungumza  na  waandishi  habari  katika  Ikulu  ya  White House, rais  wa  Marekani  Donald Trump  hakutaka  kueleza  chochote kuhusu  kujitokeza  kwa  Kim lakini  alisema , atakuwa  na  kitu  cha kusema  juu  ya  hilo katika  wakati  muafaka.

Vyombo  vya  habari  vya  taifa  viliripoti  kwamba  Kim  anafanya shughuli  za  kawaida  bila  kutoka  hadharani, kama  kutuma  salama kwa  viongozi  wa  Syria, Cuba  na  Afrika  kusini  na  kuelezea shukurani  zake  kwa  wafanyakazi  wanaojenga  maeneo  ya  kitalii katika  mji  wa  pwani wa  Wonsan, ambako  baadhi  ya  watu walisema   anaishi  huko.

Serikali  ya  Korea  kusini , ambayo  ina  rekodi  mchanganyiko za kuwafuatilia  viongozi  wa  ngazi  ya  juu  wa Korea  kaskazini , imekuwa  mara  kwa  mara  ikipuuzia  minong'ono  kuwa  Kim, anayeaminika  kuwa  na  umri  wa  miaka  36, alikuwa  katika  hali mbaya  ya  kiafya  kutokana  na  upasuaji aliofanyiwa.

Kim Yo Jong Nordkorea
Kim Yo Jong dada yake kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un Picha: Getty Images/J. Silva

Ofisi  ya  rais  Moon Jae-in  imesema  haijagundua ishara  ambazo si za  kawaida  nchini Korea  kaskazini  ama  hatua  zozote za  dharura katika  chama  tawala, jeshi ama  baraza  la  mawaziri. Seoul imesema  inaamini Kim bado  anaendesha  masuala  ya  taifa lakini anaishi  katika  eneo  ambalo  halijulikani  nje ya  Pyongyang.