1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kila unapoelekea unaikuta Ujerumani Mashariki: Kisiwa cha Berlin Magharibi

12 Agosti 2011

Kuanzia Agosti 13 mwaka 1961, hadi kufikia siku ukuta ulipoporomoka November 9 mwaka 1989, jiji la Berlin ulikuwa mji uliogawanyika. Sehemu ya magharibi wa Berlin iligeuka kuwa kisiwa cha kisiasa.

https://p.dw.com/p/12Flc
hinter der Mauer in Ostberlin und wird seit dem Mauerbau 1961 nicht mehr benutzt. Die DDR-Oberen hatten 1985 die Sprengung des abgeriegelten Gotteshauses befohlen - es stand im Todesstreifen und war den Grenzposten im Weg. Am 13. August, dem 50. Jahrestag des Mauerbaus, wird an der Bernauer Straße der zweite Abschnitt der Erinnerungslandschaft unter freiem Himmel eröffnet, zu der auch das Turmkreuz gehört. Es ist neben der Kapelle der Versöhnung aufgestellt, die auf dem Fundament der gesprengten Kirche steht und zum Gedenkensemble gehört. Foto: Chris Hoffmann dpa/lbn (zu dpa «Das verbogene Kreuz der gesprengten Kirche» vom 28.07.2011) +++(c) dpa - Bildfunk+++
Picha: picture-alliance / akg-images

Wakati sehemu ya magharibi ya Berlin ilipogeuka kuwa kisiwa, mji uliozungushwa senyenge kwa kilomita 480 za mraba. Barabara na njia kama 150 ambazo hadi ukuta ulipojengwa zilikuwa zikipitia katika maeneo yaliyokuwa yakidhibitiwa na washindi wa vita vikuu vya pili vya dunia, wakaazi wasiopungua milioni mbili wa mji huo wakawa hawawezi tena kuzitumia- zilifungwa kiufumba na kufumbua kwa kujengwa kuta, kuwekwa vizuwizi, kuzungushwa senyenge na vizuwizi vyenginevyo. Na kati ya vituo 80 vya ukaguzi vilivyokuwepo, vinne tu ndivyo vilivyokuwa vimefunguliwa.

Deutschland / DDR, Berlin: Ausbau der Grenzanlagen in der Zimmerstrasse in Kreuzberg. November 1961 Germany / GDR, Berlin. The building of the wall. Zimmerstrasse, Kreuzberg. November 1961
Picha: ullstein - Czechatz

"Hakuna mwenye azma ya kujenga ukuta." Matamshi hayo yanajulikana na kila mtu. Kiongozi wa wakati ule wa GDR Walter Ulbricht alikanusha mipango ya kutaka kujengwa ukuta. Miaka 50 iliyopita, serikali ya GDR mjini Berlin ilianza kufumba na kufumbua kuujenga ukuta. Kwa namna hiyo sio tu Ujerumani iligawika na mji wa Berlin pia ulitenganishwa. Kufumba na kufumbua pakawa sehemu ya Mashariki na ya Magharibi ya Berlin. Uamuzi wa kiholela wa kisiasa ukaacha jaraha la kina katika mji huo wa mto Spree. Kwa muda wa miaka 28 sehemu ya magharibi ya Berlin iligeuzwa kisiwa kati kati ya jamhuri ya kidemokrasi ya Ujerumani-au GDR. Katika kipindi chote hicho Berlin ya Magharibi ikawa "dunia ya walio wadogo": Lakini mji wa Berlin uligeuka kitovu cha siasa ya kimataifa. Nusu ya jiji hilo la Berlin sio tuu limetengwa kieneo na sehemu ya ardhi iliyosalia ya shirikisho basli na kisiasa pia. Mwandishi habari na mtu anaeujua vyema mji wa Berlin Wilfried Rott: "Ulikuwa wakati mgumu kwa Berlin ya Magharibi na ambao wakati huo huo ulikuwa kitambulisho cha mji huo wa magharibi kwa muda mrefu. Walikuwa na fahari kuwa wao ndio Waberlin ya Magharibi."

Wilfried Rott ameandika kitabu alichokipa jina "Die Insel" au Kisiwa, kuhusu Berlin ya Magharibi. Katika kitabu hicho anajaribu kufafanua kipi kinamfanya mtu ajitambulishe kuwa mkaazi wa Berlin ya Magharibi. "Kwamba hushughuliki na kinachotokea katika shirikisho la jamhuri ya Ujerumani. Huwezi kupiga kura. Wabunge tu wakipelekwa Bonn bila ya kupigiwa kura." Anasema.

ullstein bild - Peters Datum: 00.00.1983 Bildgröße: 2348x2202 Pixel Berlin Mauer Potsdamer Platz col Blick über die Grenzanlagen - 1983 spanische Reiter
Picha: ullstein - Peters

Berlin- kisiwa cha kisiasa kilichotengwa na sehemu iliyosalia ya shirikisho la jamhuri ya Ujerumani. Kila wakati ulipokuwa ukipita ndipo nayo sehemu ya magharibi ya Berlin ilipokuwa ikijipatia sura yake wenyewe ya utamaduni na mazingira yake wenyewe. Wanamuziki tofauti, wasanii na vijana wa kutoka kila pembe ya dunia waliamua kuhamia Berlin Magharibi. Lakini licha ya yote hayo Berlin ya Magharibi ilisalia na sura ya kimkoa: "Kwa sababu, hata kama lilikua jiji, lakini lilikuwa pia na sura ya mkoa. Hakujakuwa na vipaji vipya vya kutosha." Anasema Wilfried Rott.

Mwandishi vitabu mwengine Silvia Friedrich aliyeamua kuhamia Berlin Magharibi mwaka 1976 anasema hakuona yeye kama alikuwa akiishi mkoani. Anasema mji ulikuwa mkubwa kwa namna ambayo hawajahisi kwamba wamefungiwa. Lakini kila muda ulipokuwa ukipita na yeye pia alijisikia kama amefungwa anasema bibi Silvia Friedrich: "Angalia unapokuwa kijijini- unaweza kuendesha kama kilomita 200. Unajionea mandhari na mashamba kigodo, huku lakini haikuwa ikiwezekana. Kwasababu watu walikuwa mjini."

Kisiwa kilichokuwa kila wakati kikijitenga na sehemu yake ya mashariki. Baada ya ukuta kuporomoka wakaazi wa Berlin wakalazimika kujuana upya. Hii leo miaka 21 baada ya kuporomoka ukuta,sehemu hizo mbili za jiji la Berlin zikachanganyika upya. Berlin Magharibi ulikuwa mji wa aina yake ukulinganishwa na miji mengine ya shirikisho la jamhuri ya Ujerumani. Kwa upande mwengine lakini sehemu hiyo ya magharibi iligeuka kisiwa- kijiji kikubwa kati kati ya mfumo wa ujamaa. Kwa kuporomoka ukuta, sio tu jamhuri ya kidemokrasi ya Ujerumani-GDR imetoweka, bali pia kisiwa cha ajabu cha kisiasa ambacho njia zake zote zilikuwa zikielekea mashariki, hakipo tena.

Miaka 50 baada ya kujengwa ukuta wa Berlin Agosti 13 mwaka 1961, Berlin inajitahidi kuhifadhi mabaki ya ukurasa huo mweusi wa historia yake. Mabaki ya ukuta yanahifadhiwa na kutunzwa kwa lengo la kutuliza kiu cha watalii na vizazi vijavyo. "Mambo hayakuwa hivi. Mwanzoni mwa miaka ya 90, asilimia 90 ya wakaazi wa Berlin walitaka kwa kila hali kutokomeza ukuta", anasema Rainer Klemke anaeshughulikia masuala ya utamaduni katika serikali ya jiji la Berlin. Anakumbuka furaha iliyofuatia kuporomoka ukuta wa Berlin November 9 mwaka 1989 na hofu ya wakaazi kuuona ukifungika tena. Baadae katika miaka ya 200 wakaazi wa Berlin wakaanza kujiuliza kilichotokea- anajikumbusha Rainer Klemke na akuongezea tangu wakati huo ndipo ilipozuka fikra ya kuhifadhiwa ukuta wa Berlin mpango ulioidhinishwa mwaka 2006 na muungano wa vyama tawala katika serikali ya muungano wa vyama vya mrengo wa shoto katika jiji la Berlin.

Vituo vya ukaguzi vya Charlie- kitambulishi cha vita baridi, lango la Brandenburg- kitambulisho cha mtengano na muungano na Bernauer Strasse eneo lililokuwa likitumiwa na wengi waliokuwa wakikimbia Ujerumani Mashariki, na kulikojengwa mahndani mengi zaidi ni maeneo yanayopendwa sana kutembelewa na watalii. Mwaka jana kituo cha Makumbusho cha Bernauer kilitembelewa na zaidi ya watu laki tano, wengi wakiwa ni wanafunzi- idadi kubwa kabisa ikilinganishwa na watalii lati tatu waliolitembeleya eneo hilo mwaka 2009.

Mwandishi: Klemm,Franziska/Hamidou Oummilkheir

Mhariri: Abdul-Rahman, Mohammed