1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHaiti

Kikosi cha polisi wa Kenya kuelekea Haiti Juni 25

24 Juni 2024

Kikosi cha polisi wa Kenya kitaondoka kuelekea Haiti hapo kesho Jumanne (Juni 25) ili kuongoza ujumbe unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa kukabiliana na ghasia za magenge katika nchi hiyo ya Caribbean.

https://p.dw.com/p/4hPno
Kenya | Polisi wakijaribu kuzima maandamano huko Kibera, Nairobi
Maafisa wa Polisi wa Kenya wakijaribu kuzima maandamano huko Kibera jijini Nairobi: 19.07.2023Picha: Brian Inganga/AP Photo/picture alliance

Kenya ilijitolea kutuma takriban polisi 1,000 watakaoungana na vikosi kutoka nchi nyingine ili kusaidia  kuleta utulivu nchini Haiti,  lakini hatua hiyo ilikabiliwa na changamoto za kisheria katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Rais William Ruto amekuwa akiunga mkono hatua hiyo ambayo inatiliwa mashaka na shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu la Human Rights Watch hasa kuhusu ufadhili wake.

Soma pia: Rais Ruto wa Kenya asisitiza kupeleka polisi nchini Haiti wiki chache zijazo

Mbali na Kenya, nchi nyingine ambazo zimeonyesha nia ya kujiunga na ujumbe huo wa kulinda amani Haiti ni pamoja na Benin, Bahamas, Bangladesh, Barbados na Chad.