1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kijana wa pili athibitishwa kufa maandamano ya Kenya

Sylvia Mwehozi
22 Juni 2024

Tume ya Haki za Binadamu ya Kenya imethibitisha kifo cha kijana wa pili, aliyefariki wakati wa maandamano ya wiki hii nchini humo. Maandamano hayo yalianza Jumanne katika mji mkuu wa Nairobi kabla ya kuenea nchi nzima.

https://p.dw.com/p/4hOGc
Kenya | Maandamano |Nairobi
Waandamanaji jijini NairobiPicha: LUIS TATO/AFP/Getty Images

Tume ya Haki za Binadamu ya Kenya imethibitisha kifo cha kijana wa pili, aliyefariki wakati wa maandamano ya wiki hii nchini humo. Kulingana na msemaji wa Tume ya Haki za Binadamu ya Kenya Ernest Cornel, kijana mwenye umri wa miaka 21 aliyetambulika kwa majina ya Evans Kiratu alikufa baada ya kupigwa na bomu la machozi wakati wa maandamano. Kijana huyo alikimbizwa hospitali siku ya Alhamisi kabla ya kufikwa na umauti.

Soma: Mtu mmoja auawa, zaidi ya 200 wajeruhiwa maandamano ya Kenya

Maandamano hayo yaliyoongozwa kwa kiasi kikubwa na vijana na kurushwa moja kwa moja kupitia mitandao, yanapinga nyongeza za kodi na sera za kiuchumi za Rais William Ruto. Maandamano hayo yalianza siku ya Jumanne katika mji mkuu wa Nairobi kabla ya kuenea nchi nzima. Waandamanaji wameitisha maandamano mengine ya nchi nzima Juni 25.