KIGALI:Waasi wa FDLR wawekewa muda wa mwisho kusalimisha silaha
25 Agosti 2005Matangazo
Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo,Rwanda pamoja na Uganda leo zimewapa muda wa mwezi mmoja waasi wakihutu wa warwanda mashariki mwa Kongo kuweka chini silaha na kurejea nchini kwa mujibu wa mkataba uliofikiwa mapema mwaka huu.
Maafisa wa nchi hizo tatu wanaokutana mjini Kigali Rwanda wamefanya mazungumzo na kuwapa muda hadi mwishoni mwa mwezi Septemba wanajeshi waasi wa FDLR kuzingatia mkataba wa rome la sivyo huenda wakachukuliwa hatua kali.
Serikali ya Kigali inawashutumu waasi hao ambao inadai wengi wao walihusika moja kwa moja kwenye mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 nchini Rwanda.
Waasi hao wametoa masharti kadha ili waweze kurudi Rwanda.