1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIGALI:Ufaransa na Rwanda zarejesha uhusiano wa kidiplomasia

31 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBdQ

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Bernard Kouchner anapanga kuzuru nchi ya Rwanda hivi karibuni katika juhudi za kurejesha uhusiano wao wa kidiplomasia.Hayo ni kwa mujibu wa Waziri anayehusika na masuala ya ushirikiano wa kikanda Rosemary Museminali.Hakuna maelezo zaidi yailiyotolewa kuhusu ziara hiyo.

Rwanda ilivunja uhusiano wake wa kidiplomasia na Ufaransa Novemba mwaka jana baada ya jaji mmoja wa Kifaransa Jean-Louis Brugiere kutoa hati za kukamtwa kwa wasaidizi wa karibu wa Rais Paul Kagame kuhusiana na kesi ya mauaji ya kiongozi wa taifa hilo Juvenal Habyarimana yaliyopelekea mauaji ya mwaka 94 kutokea.

Rwanda kwa upande wake inalaumu Ufaransa kwa kuunga mkono wapiganaji wa Kihutu walioendesha mauaji hayo vilevile kusuasua katika kushirikiana nao kuwashataki wahusika.