1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kigali. Waziri wa zamani afungwa.

13 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEbm

Mahakama moja nchini Rwanda jana imemhukumu waziri wa zamani wa nchi hiyo kwenda jela miaka mitano kwa kuhusika na rushwa.

Hakimu Judith Mbabazi wa mahakama ya mjini Kigali alimpata na hatia Patrick Habamenshi, waziri wa zamani wa kilimo na mifugo, kwa kuhusika na ubadhirifu wa kiasi cha dola 65,000 wakati akiwa waziri.

Habamenshi, ambaye pia ana hati ya kusafiria ya Canada , alifukuzwa kazi mapema mwaka huu kwa madai ya ulaji rushwa yaliyotolewa na vyombo vya habari vya nchi hiyo dhidi yake.

Waendesha mashtaka wamemshutumu kwa kuendea kinyume utaratibu wa zabuni mwaka jana wakati alipoichagua kampuni moja nchini humo na kuilipa mamilioni ya fedha zilizotolewa na wafadhili ili kutayarisha sera ya kilimo nchini Rwanda.