1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIGALI: Vikosi vya Rwanda kusaidia nchini Sudan

5 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFZQ

Rwanda ipo tayari kupeleka vikosi vyake nchini Sudan kama sehemu ya tume ya Umoja wa Mataifa. Baada ya makubaliano ya amani kutiwa saini kuvimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu miaka 21,Umoja wa Mataifa unatazamia kupeleka vikosi vyake kusimamia amani.Afisa wa ngazi ya juu katika jeshi la Rwanda ameliambia shirika la habari AFP kuwa Rwanda imeombwa kupeleka wanajeshi 200 kufungua makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini Khartoum na katika mji wa kusini Juba.Mwezi January serikali ya Khartoum na waasi wa kusini mwa nchi-SPLA waliokuwa wakipigana tangu mwaka 1983 walitia saini mapatano ya amani kusitisha mapigano.