1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIGALI-Shirika la Chakula la UM kupunguza mgao wa chakula kwa silimia 30 kwa wakimbizi waliopo kambini Rwanda.KIGALI:

24 Februari 2005
https://p.dw.com/p/CFb8

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula-WFP,limeonya kuwa litalazimika kupunguza mgao wa chakula kwa wakimbizi 50,000 wanaotoka Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo katika kambi zao zilizopo nchini Rwanda,iwapo wafadhali hawatajitolea kuongeza kiasi cha dola milioni 2.6 za msaada.

Shirika hilo limesema kuwa iwapo fedha hizo hazitapatikana itawalazimu kukata kwa silimia 30 kiwango cha chakula wanachotoa kwa wakimbizi hao,ambao idadi yao imekuwa ikiongezeka kufuatia mapigano ya hivi karibuni na kuzorota kwa hali ya usalama mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Kwa sasa idadi ya wakimbizi waliokatika kambi sita nchini Rwanda ni 50,000 ikiwa ni wakimbizi 15,000 zaidi ya wale wanaokusudiwa kuwepo katika kambi hiyo na wote wanategema kwa kila hali kupatiwa msaada wa chakula la shirika hilo kwa sababu wamekatazwa kutafuta ajira yoyote ile.