1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kigali. Kiongozi wa kanisa ahojiwa mahakamani kuhusiana na mauaji ya 1994.

23 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CErc

Kiongozi wa kanisa katoliki nchini Rwanda ametoa ushahidi katika mahakama ya kijiji siku ya Alhamis kuhusiana na yeye kuhudhuria mikutano , watu walionusurika wanasema ilifanyika ili kupanga mauaji hayo ya halaiki mwaka 1994.

Askofu mkuu Thaddee Ntihinyurwa, ambaye ni Mhutu , aliitwa katika mahakama hiyo baada ya watu kadha ambao wamenusurika katika mauaji hayo kumshutumu Askofu huyo kwa kushiriki katika mikutano kadha wanayosema ilifanyika kupanga mauaji ya Watutsi katika jimbo la kusini la Cyangugu.

Wakiristo wa madhehebu ya kikatoliki wamekuwa wakishutumiwa kwa kuhusika na mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 ambapo watu wenye msimamo mkali kutoka katika kabila kubwa la Wahutu waliwauwa Watutsi 800,000 ambao ni kabila dogo , pamoja na Wahutu waliochukua msimamo wa kati katika siku 100 za mauaji hayo.