1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIGALI. Clinton akamilisha ziara barani Afrika

24 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CErP

Aliyekuwa rais wa Marekani Bill Clinton alitoa masikitiko yake na kukiri kuwa hakuwajibika vilivyo wakati alipokuwa rais ili kuzuia mauaji ya nchini Rwanda ya mwaka 1994 ambapo watu laki 8 waliuwawa kinyama.

Bwana Clinton aliyasema hayo baada ya kuweka shada la maua katika makavazi yenye kumbukumbu ya wahanga wa mauaji ya Rwanda wakati wa ziara fupi nchini humo iliyoazimia kuzuru miradi ya UKIMWI.

Nchi ya Rwanda ndio ilikamilisha ziara ya bwana Clinton ya mataifa sita ya Afrika kujionea jinsi ugonjwa wa UKIMWI unavyo waathiri watoto kutoka bara linalokabiliwa na umasikini mkubwa ulimwenguni.