1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIEV Ukraine yataka kujiunga na umoja wa Ulaya.

18 Februari 2005
https://p.dw.com/p/CFce

Rais wa Ukraine, Viktor Yuschenko, amesema katu hatokubali taifa lake liwe mshiriki wa jumuiya ya Ulaya na badala yake akasisitiza anataka Ukraine ijiunga na umoja huo mwaka wa 2007. Akizunguza kabla ziara yake rasmi Jumatatu ijayo mjini Brussles Ubelgiji, Yuschenko amesema mazungumzo yake na maafisa wa umoja wa Ulaya yatatuwama juu ya kuweka tarehe ya kuanza mjadala wa kuiruhusu Ukraine kuwa mwanachama. Wakati wa ziara ya Yuschenko, umoja wa Ulaya utaidhinisha mpango utakaolifaidi taifa hilo kibiashara na kulegezwa kwa sheria za utoaji visa za kusafiria. Hata hivyo mpango huo hausemi ikiwa umoja huo utaliunga mkono pendekezo la Ukraine la kutaka kujiunga na jumuiya hiyo.