1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM:Jopo juu ya kifo cha Garang kutembelea eneo la ajali

17 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEkR

Jopo linalochunguza kifo cha makamu wa kwanza wa rais wa Sudan John Garang hapo kesho linatarajiwa kutembelea eneo kulikoanguka ndege iliyokuwa imembeba kiongozi huyo.

Jopo hilo litafika hadi mjini Kampala Uganda ambako litakutana na makundi mengine yanahusika katika kuchunguza ajali hiyo.

Serikali ya Sudan imesema itakubali usaidizi kutoka nchi yeyote ile katika uchunguzi ambapo tayari Marekani,Uingereza,Kenya na Umoja wa Mataifa umejitolea

Kusaidia.

Marehemu Garang alifariki mwezi Juli 30 baada ya helikopta ya rais Museveni wa uganda iliyokuwa imembeba kumrejesha Kusini mwa Sudan kuanguka .