1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM : Kikosi cha Umoja wa Mataifa kushambuliwa

15 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDLL

Rais Omar al Bashir ameonya kwamba Sudan itakabiliana na vikosi vyo vyote vile vitakavyodhaminiwa na Umoja wa Mataifa vitakavyotumwa katika eneo lililoathirika na vita la Dafur na kwamba watapambana navyo kama vile Hizbollah ilivyovipiga vikosi vya Israel nchini Lebanon.

Bashir ameviambia vikosi vilivyokusanyika kusini mwa mji mkuu wa nchi hiyo hapo jana kuadhimisha miaka 52 ya jeshi la Sudan kwamba wanayakinisha msimamo wao huo kwa vikosi vya kimataifa vitakayvoingia Dafur.

Rais huyo wa Sudan amesema wanapinga kuwekwa kwa nguvu kwa wanajeshi wa Marekani,Uingereza au wanajeshi wengine na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Amewapongeza Hizbollah kwa kuvunja mwiba wa jeshi la Israel milele.