1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM: Azimio la Umoja wa Mataifa limekosolewa na Sudan

2 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFR2

Serikali ya Sudan imelishutumu azimio la Umoja wa Mataifa linalotaka watuhumiwa wa uhalifu wa vita katika jimbo la Darfur wafikishwe mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu mjini The Hague.Waziri wa habari wa Sudan,Abdel Basit Sabdarat amewaambia waandishi wa habari mjini Khartoum kuwa mahakama hiyo inakiuka kanuni ya taifa ya kujiamulia yenyewe mambo yake.Lakini makundi mawili makuu ya waasi katika jimbo la Darfur yamelikaribisha azimio hilo na kusema kuwa yatatekeleza maamuzi yake.Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio hilo kwa kura 11 kwa 0.Marekani na nchi tatu zingine hazikupiga kura.Marekani ambayo huipinga Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu haikutumia kura yake ya turufu.Azimio lililopitishwa linahusika na orodha ya watu 51 kushtakiwa katika Mahakama ya The Hague,wakituhumiwa kuhusika na uhalifu dhidi ya ubinaadamu katika jimbo la Darfur magharibi mwa Sudan.