1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Khan: Hakuna nafasi tena ya kutetereka

27 Februari 2023

Mkuu wa Bayern Munich Oliver Khan amewaonya wachezaji wa klabu hiyo kutofanya makosa zaidi baada ya kupata ushindi wa 3-0 dhidi ya Union Berlin, moja ya washindani wao wakubwa wa kuwania ubingwa wa Bundesliga msimu huu.

https://p.dw.com/p/4O1sD
Bundesliga | FC Bayern München v 1. FC Union Berlin | Thomas Müller und Jamal Musiala
Picha: CHRISTOF STACHE/AFP

Borussia Dortmund walikuwa wamekwea hadi kileleni mnamo Jumamosi baada ya kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya TSG Hoffenheim ila sasa wanajikuta katika nafasi ya pili wakiwa na pointi sawa na Bayern, 46 ila wanadunishwa na uchache wa magoli.

Kocha Julian Nagelsmann amesema kuwa amefurahia jinsi vijana wake walivyofunga magoli ya mapema katika kipindi cha kwanza na kuwavunja moyo wapinzani wao.

Union Berlin wamefanya miujiuza hata kuwa miongoni mwa timu zinazopigania ubingwa kwa kuwa walipandishwa daraja tu mwaka 2019 na hawana utajiri wa miamba kama Bayern Munich.

Kocha wa Union Urs Fischer amekiri kwamba kimchezo, Bayern walikuwa hatua mbili au tatu juu yao.