Khamenei asema hakuna chohote kibaya na mpango wa nyuklia
11 Juni 2023Matangazo
Hayo ni wakati kukiwa na mkwamo kati ya Tehran na Washington wa kuufufua muafaka wa nyuklia wa mwaka wa 2015.
Soma pia: IAEA yatatua masuala ya nyuklia na Iran
Khamenei amesema hakuna chochote kibaya na makubaliano na nchi za Magharibi lakini miundo mbinu ya sekta ya nyuklia ya nchi hiyo haipaswi kuguswa. Amesema tuhuma kuwa Tehran inatengeneza silaha za nyuklia ni za uwongo.
Khamenei ameongeza kuwa hawataki silaha za nyuklia kwa sababu ya imani zao za kidini.
Miezi kadhaa ya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Tehran na Washington ya kuyafufua makubaliano hayo ya Nyuklia na madola sita yenye nguvu duniani yamekwama tangu Septemba, huku pande zote zikimtuhumu mwenzake kwa kuweka masharti yasiyowezekana.