1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiUjerumani

Kesi ya udanganyifu wakati wa COVID yasikilizwa Ujerumani

Angela Mdungu
11 Agosti 2023

Mahakama ya Cologne nchini Ujerumani, leo imeanza kusikiliza kesi ya udanganyifu wa takribani Euro milioni 16, inayowakabili wanaume watatu.

https://p.dw.com/p/4V4K8
Coronavirus - Testzentrum
Picha: Bernd Weißbrod/dpa/picture alliance

Wanaume hao, kupitia kutumia kampuni bandia wanadaiwa kufungua vituo 10 vya kupimia virusi vya korona, katika miji ya Cologne na Langenfeld waliilidanganya shirika la umma la bima ya afya la Nordrhein  na kulipwa fedha hizo.

Kulingana na mwendesha mashitaka watuhumiwa hao waliamua kujinufaisha kupitia mchakato wa malipo ambao haukuwa na urasimu mwezi Juni 2021 na kudai malipo hayo kwa shirika hilo la bima ya afya.

Walifungua akaunti za mtandaoni kwa kutumia majina ya watu wengine ambao raia wa Italia kwa ajili ya malipo ya vituo hivyo ambavyo havipo.

Walifanya hivyo kwa kudai malipo ya vipimo ambavyo havikuwahi kufanyika. Walitumia namba za vituo vingine vilivyoandikishwa kudai malipo.

Mshtakiwa wa tatu kwenye kesi hiyo anadaiwa kusaidia uhalifu  huo kwa kuweka masanduku ya barua ya vituo hivyo bandia mitaani. Kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa kwa mara nyingine kumi na saba na hukumu inatarajiwa kusomwa mwisho wa mwezi Oktoba