1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kesi ya rufaa ya Julian Assange kusikilizwa mjini London

20 Februari 2024

Kesi ya mwisho ya rufaa ya mwanzilishi wa tovuti ya WikiLeaks Julian Assange imeanza kusikilizwa mjini London, Uingereza.Wakili wa Assange Edward Fitzgerald amesema mashtaka ya mteja wake hayawezi kuthibitishwa.

https://p.dw.com/p/4cdBc
Kroatien | Proteste Unterstützer von Julian Assange in Zagreb
Maandamano ya kupinga Assange kurejeshwa Marekani yafanyika huku kesi yake ikianza kusikilizwa mjini London.Picha: Damir Sencar/AFP

Assange mwenye umri wa miaka 52 na raia wa Australia hakuweza kuhudhuria kesi yake itakayosikilizwa kwa siku mbili, kutokana na maradhi.

Mwanaharakati huyo anapinga kurejeshwa nchini Marekani ili kujibu mashtaka ya kuchapisha nyaraka za siri za kijeshi na kidiplomasia zinazohusu vita vya Marekani katika mataifa ya Iraq na Afghanistan.

Bunge la Australia lataka muasisi wa WikiLeaks arejeshwe

Stella Assange amesema ikiwa itahitajika, mume wake ataiomba Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu kusitisha kwa muda uamuzi huo, akionya kuwa mumewe yuko hatarini kufa iwapo atarejeshwa Marekani.