1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kesi ya mpiganaji wa jihadi kutoka Mali yasikilizwa ICC

14 Julai 2020

Kesi ya mpiganaji wa jihadi Mali anayeshitakiwa kwa kuharibu maeneo ya ibada mjini Timbuktu na kuanzisha  utawala wa ukandamizaji na mateso inaanza kusikilizwa Jumanne katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).

https://p.dw.com/p/3fHjY
Al-Hassan Ag Abdoul Aziz Ag Mohamed Ag Mahmoud
Picha: AFP/E. Plevier

Al-Hassan ag Abdoul Aziz Mohamed Ag Mahmoud, mwenye umri wa miaka 42, ameshitakiwa kwa   uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya ubinadamu, ubakaji na utumwa wa kingono.

Mashitaka hayo yanaanzia wakati kundi la Waislamu wenye itikadi kali walipotumia mapambano ya  kundi la kabila la Tuareg mwaka 2012 kuikamata miji iliyoko katika hali tete upange wa kaskazini nchini  Mali.

Waendesha mashitaka katika mahakama mjini The Hague watatoa maelezo yao ya ufunguzi dhidi ya  mtu waliyemwelezea katika kikao cha kabla kuwa aliwatesa sana wakaazi wa eneo hilo.