1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kesi kuhusu mauwaji nchini Rwanda yaaakhirishwa Tanzania:

26 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CFxt
DAR ES SALAAM: Maafisa wane wa zamani wa Rwanda wanafikishwa mahkamani hiyo kesho kwa mashtaka walichangia mno mauwaji ya mwaka 1994 ya watu laki nane, pakiwamo utoaji mafunzo kwa wanamgambo, na kuandaa orodha ya watu wa kuuawa. Hii ni kesi ya pili mwezi huu kuhusiana na mawaziri na mafisa wa ngazi za juu wa zamani nchini Rwanda, kwa tuhuma walichochea chuki za kikabila na mauwaji. Msemaji wa Mahkama ya Umoja kwa ajili ya Rwanda, ROLAND AMOUSSOUGA, alisema kesi hiyo ni muhimu, hasa inahusika na mchango wa mawaziri na maafisa wa zamani wa serikali. Kesi ilitarajiwa kufunguliwa leo, lakini imeahirishwa hadi kesho kutokana na uamuzi wa Tanzania kwamba leo waislamu wanasherehekea IDIL FITR, kumalizika kwa funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhan.