1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiUjerumani

Kesi dhidi ya mshukiwa wa mauaji Ujerumani yaanza

Josephat Charo
24 Oktoba 2023

Mwanamume wa umri wa miaka 27 aliyewadunga kisu watu kadhaa na kuwaua wawili katika mji wa Duisburg nchini Ujerumani amepandishwa kizimbani.

https://p.dw.com/p/4XwQK
Mwanamume aliyewadunga kisu watu kadhaa na kuwaua wawili katika mji wa Duisburg nchini Ujerumani amefikishwa mahakamani
Mwanamume aliyewadunga kisu watu kadhaa na kuwaua wawili katika mji wa Duisburg nchini Ujerumani amefikishwa mahakamaniPicha: Christoph Reichwein/dpa/picture alliance

Mshukiwa huyo, mhamiaji kutoka Syria, ameshtakiwa kwa mauaji na anakabiliwa na mashitaka matatu ya majaribio ya kuua.

Waendesha mashitaka wa shirikisho katika mahakama ya juu ya Dusseldof wamewasilisha hoja wakisema mashambulizi hayo ya kisu yalichochewa na msimamo wa kidini.

Waendesha mashitaka pia wamesema mshukiwa anajiona kama shahidi wa kundi la kigaidi linalojiita dola la kiislamu, akipania kuua watu wengi kadri inavyowezekana. Mahakama ya Dusseldorf imepanga siku 18 za kusikilizwa kwa kesi hiyo hadi Januari 2024.