1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenyatta atoa wito wa kupunguza mzozo DR Kongo

25 Januari 2023

Rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta ametoa wito wa kukomeshwa kwa mgogoro Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

https://p.dw.com/p/4Mh2v
DR Kongo Kenias ehem. Präsident Uhuru Kenyatta in Goma
Picha: Benjamin Kasembe/DW

Rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta ametoa wito wa kukomeshwa kwa mgogoro Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambao matatizo yake yanayozidi kila kukicha yamechochea mvutano wa kidiplomasia kati ya DRC na Rwanda.

Kenyatta ni mmoja ya wapatanishi katika mzozo huo kwa niaba ya nchi saba wanachama wa Umoja wa Afrika Mashariki.

Ameelezea wasiwasi wake juu ya hali inayozidi kuwa mbaya katika eneo la Kivu Kaskazini ambako mapigano makali yamekuwa yakiripotiwa kati ya makundi yaliojihami kwa silaha, wanajeshi wa serikali na kundi la M23.

Taarifa ya Kenyatta imetolewa siku moja baada ya Rwanda kuishambulia ndege ya kivita ya Congo kwa madai ya kukiuka sheria na kuingia katika anga yake.