1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya yathibitisha kisa cha kwanza cha Corona

Shisia / MMT13 Machi 2020

Kisa cha kwanza cha virusi vya Corona kimeripotiwa nchini Kenya. Wizara ya Afya nchini humo imesema kuwa kisa hicho kilithibitishwa siku ya Alhamisi kwa raia wa taifa hilo aliyesafiri kutoka Marekani akirejea nyumbani. Waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema mgonjwa huyo amewekwa kwenye karantini na yuko katika hali nzuri. Sikiliza ripoti ya Shisia Wasilwa

https://p.dw.com/p/3ZLlO