1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya yakabiliwa na kitisho cha njaa, ripoti

10 Februari 2023

Kenya imejikuta kwenye nafasi ya 94 kati ya mataifa 121 kwenye tathmini mpya ya hali ya njaa ya ulimwengu.

https://p.dw.com/p/4NL74
Kenia Dürre l Kadaver einer Kuh, im Hintergrund Turkana-Frauen mit Feuerholz
Picha: Simon Maina/AFP

Kwa mantiki hii, alama 23.5 zinaliweka taifa hilo katika hali mahututi. Jumla ya mataifa 44 yako katika hali ya kutisha mintarafu njaa. Wakati huohuo, serikali ya Kenya inasaka misaada ya ziada kukidhi mahitaji ya watu milioni 5.3 wanaokabiliana na njaa ana kwa ana.

Kulingana na tathmini hiyo mpya iliyotangazwa Ijumaa jijini Nairobi, juhudi za kupambana na njaa kote ulimwenguni zimesuasua katika miaka ya hivi karibuni.

UN: Watu milioni 22 wakabiliwa na njaa pembe ya Afrika

Viashiria vilivyotumiwa ni pamoja na utapia mlo, unyaufu na kudumaa ni changamoto zinazowakumba watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.Mwaka 2021, kiasi ya watu milioni 828 walitatizwa na utapia mlo.

Hali hiyo huenda ikawa mbaya zaidi ukizingatia majanga ya kidunia kama vile migogoro, mabadiliko ya tabia ya nchi na vurugu za kiuchumi kufuatia madhila ya covid 19.

Ongezeko la bei za bidhaa za vyakula, mafuta na mbolea hali ambayo itachangia kwa kiasi kikubwa uhaba wa chakula.
Ongezeko la bei za bidhaa za vyakula, mafuta na mbolea hali ambayo itachangia kwa kiasi kikubwa uhaba wa chakula.Picha: DW/Michael Kwena

Akipokea rasmi ripoti ya hali ya njaa ya mwaka 2022 kwa Kenya, Waziri Kiongozi Musalia Mudavadi aliwasisitizia wadau kuhusu umuhimu wa kusaka suluhu mujarab za kupambana njaa.

Marsabit wataka chakula cha misaada kisitishwe

Kimataifa, vita vya Ukraine vimeusukuma ulimwengu pembeni na kusababisha ongezeko la bei za bidhaa za vyakula, mafuta na mbolea hali ambayo itachangia kwa kiasi kikubwa uhaba wa chakula kwa jumla kwa mwaka huu na baadaye.

Tathmini ya njaa ya mwaka 2022 inabainisha kuwa mataifa ya Afrika yaliyo kusini mwa jangwa la Sahara pamoja na kusini mwa Asia, ndiyo maeneo ambayo yaliyo na idadi kubwa zaidi ya watu wanaotatizwa na njaa na walio hatarini zaidi kuathiriwa na majanga na misukosuko.

Kwa sasa, serikali ya Kenya imezindua mkakati wa kuufufua uchumi wake utakaozichagiza sekta za maendeleo na kuukuza uchumi.
Kwa sasa, serikali ya Kenya imezindua mkakati wa kuufufua uchumi wake utakaozichagiza sekta za maendeleo na kuukuza uchumi.Picha: Kossivi Tiassou/DW

Bila ya mabadiliko ya msingi,si tuu ulimwengu mzima au mataifa yasiyopungua 46 yanatazamiwa kuvishusha viwango vya njaa na kuitokomeza ifikapo mwaka 2030.

Ukame waua tembo 205 nchini Kenya

Kwa sasa, serikali ya Kenya imezindua mkakati wa kuufufua uchumi wake utakaozichagiza sekta za maendeleo na kuukuza uchumi.

Mwanzoni mwa wiki hii naibu wa rais Rigathi Gachagua aliwarai wadau na wafadhili kuimarisha juhudi za kukidhi mahitaji ya wakenya wanaokabiliana na njaa.

Tathmini hiyo ya hali ya njaa ulimwenguni imeandaliwa na mashirika ya misaada ya WeltHunger Hilfe ya Ujerumani na Concern Worldwide la Ireland linalolenga kupunguza umasikini.

Mwandishi: Thelma Mwadzaya, DW Nairobi