1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waliofariki wafikia 6 kufuatia mlipuko wa gesi Kenya

5 Februari 2024

Idadi ya waliofariki kutokana na mlipuko wa gesi jijini Nairobi nchini Kenya wiki iliyopita, imeongezeka na kufikia watu sita.

https://p.dw.com/p/4c2OW
Kenya | Mlipuko wa Gesi jijini Nairobi
Afisa wa Polisi akishuhudia lori la gesi lililoteketea kwa moto baada ya mlipuko huko Embakasi jijini Nairobi: 02.02.2024Picha: Luis Tato/AFP/Getty Images

Hayo ni kulingana na Msemaji wa serikali ya Kenya Isaac Maigua Mwaura ambaye ameeleza pia kuwa kati ya watu 280 waliojeruhiwa, 53 bado wanapokea huduma katika hospitali mbili za Nairobi.

Soma pia: Kenya yasema rushwa ndio imechangia mlipuko wa gesi

Lori lililokuwa limebeba mitungi ya gesi lililipuka Alhamisi usiku huko Embakasi, wilaya yenye wakazi wanaokadiriwa kufikia milioni 1, na kusababisha maafa na uharibifu mkubwa. Polisi wamesema msako bado unaendelea kumtafuta mmiliki wa biashara hiyo.