1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Marekani yaadhimisha miaka 22 tangu mashambulizi ya kigaidi

11 Septemba 2023

Marekani leo inafanya kumbukumbu ya miaka 22 tangu kutokea mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11 mwaka 2001 yaliyoitikisa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4WCyy
Baadhi ya watu wakitoa heshima zao katika maadhimisho ya kuwakumbuka wahanga wa mashambulizi ya kigaidi nchini Marekani, Septemba 11, 2001
Baadhi ya watu wakitoa heshima zao katika maadhimisho ya kuwakumbuka wahanga wa mashambulizi ya kigaidi nchini Marekani, Septemba 11, 2001Picha: Yuki Iwamura/AP/dpa/picture alliance

Marekani ilijibu mashambulizi hayo kwa hatua nzito zilizokuwa na taathira pana katika kila pembe ya dunia.

Mjini New York, kengele ziligongwa kwenye viunga yalipokuwepo majengo pacha ya ghorofa ya Kituo cha Kimataifa cha Biashara, ambayo yaliporomoka baada ya magaidi kuyashambulia kwa kutumia ndege mbili za abiria walizoziteka nyara.

Ndege nyingine iliangushwa kwenye majengo ya wizara ya ulinzi, Pentagon na ya nne ilianguka huko Pennsylvania baada ya mapambano kati ya abiria na watekaji nyara.

Shughuli za kumbukumbu na kutoa heshima kwa zaidi ya watu 3,000 waliopoteza maisha wakati wa shambulio hilo zimefanyika pia kwenye maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.

Rais Joe Biden aliye njiani kurejea nyumbani akitokea ziarani barani Asia anatarajiwa kushiriki moja ya mikusanyiko ya kumbukumbu kwenye kambi moja ya kijeshi.