1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUingereza

Keir Starmer aanza majukumu kama Waziri Mkuu wa Uingereza

5 Julai 2024

Keir Starmer ameanza majukumu ya kuwa waziri mkuu mpya wa Uingereza baada ya kupokea baraka za mfalme Charles wa tatu kuunda serikali ijayo.

https://p.dw.com/p/4hw7T
Uchaguzi wa Bunge la Uingereza | Waziri Mkuu mpya wa Keir Starmer
Waziri Mkuu mpya wa Uingereza Keir Starmer akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) mbele ya ofisi yake ya Downing Street 10Picha: Phil Noble/REUTERS

Akizungumza baada ya kukutana na mfalme Charles III katika kasri la Buckingham, Starmer alimshukuru waziri anayeondoka Rishi Sunak.

 "Nataka kumshukuru waziri mkuu anayeondoka Rishi Sunak, mafanikio yake kama waziri mkuu wa kwanza mwenye asili ya Asia nchini Uingereza. Juhudi zake za ziada hazipaswi kupuuzwa na mtu yoyote.''

Starmer anakuwa waziri mkuu baada ya chama chake cha Labour kupata ushindi wa kishindo ambao umekitikisa chama cha Conservative kwa kukipokonya viti vingi vilivyokuwa vinashikiliwa na mawaziri wake ikiwemo cha aliyewahi kuwa waziri mkuu, Liz Truss.