1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vipimo vyachelewa huku maambukizi yakishika kasi Marekani

Angela Mdungu
15 Julai 2020

Wakati idadi ya maambukizi ya virusi vya corona nchini Marekani ikipindukia milioni tatu nchini Marekani, wataalamu wa afya wamesema kutokana na upimaji usiokidhi, maambukizi yasiyo na dalili kali yanakosa kuripotiwa.

https://p.dw.com/p/3fN7S
USA Texas Coronavirus Maßnahmen
Picha: picture-alliance/dpa/U.S. National Guard

Licha ya idadi kubwa ya maambukizi na zaidi ya vifo 130,000 tangu kuingia kwa janga hilo nchini Marekani, wananchi wa taifa hilo wamekuwa wakikabiliwa na misururu mirefu na joto kali kuelekea kwenye vituo vya upimaji wa virusi hivyo huku kukiwa na hatari ya ongezeko la maambukizi.

Watu wengine wamekuwa wakienda kwenye vituo vya upimaji kwa zaidi ya wiki bila kupata majibu yao. Baadhi ya vituo vinapungukiwa na vipimo wakati maabara zikiripoti uhaba wa vifaa na wafanyakazi wa kufanya vipimo vya corona.

Baadhi ya Wamarekani waliochanganyikiwa kutokana na hali hii wamebaki wakishangaa ni kwa nini taifa lao inashindwa kuchukua hatua madhubuti, hasa ikiwa lilishapewa onyo wakati virusi hivyo vilipoleta madhara nchini China, Italia Uhispania na mjini New York.


Mmoja wa raia nchini Humo anayetokea Austin, Texas Sam Lee anasema alijaribu kufanyiwa vipimo vya covid 19mara tatu, mwezi uliopita. Hii ni kutokana na kupatwa na kikohozi, kuishiwa pumzi mara tatu mwezi uliopita. Kwa mara ya kwanza alikwenda kwenye kituo cha upimaji saa moja kabla ya wa vipimo.

USA Coronavirus Donald Trump PK
Rais wa Marekani Donald Trump akionyesha orodha ya vituo vya upimaji wa virusi vya Corona, ambavyo anasema Marekani inaweza kuvitumia kubaliana na kasi ya mambukizi.Picha: Reuters/J. Ernst

Aliambiwa kituo kilikuwa kikipanga kufungwa na kwamba kimejaa. Alikataliwa tena katika kituo cha pili baada ya mvua kusababisha kufungwa kwa kituo hicho. Kwenye kituo cha tatu, Lee aliamua kuondoka mwenyewe baada ya mtu mmoja mbele yake kumwambia kuwa wamekuwa wakisubiri kwa zaidi ya saa tatu.

Soma zaidi WHO: Maambukizi ya virusi vya corona yaongezeka ulimwenguni 

Kwa upande wake Jennifer Hudson, 47, wa Tuscon Arizona anasema hili ni tatizo kubwa. "Ukweli kwamba tunayategemea makampuni na hakuna mrejesho kutoka serikalini ni suala la ajabu. Inasababisha watu wanaostahili vipimo kukosa vipimo.

Alitumia siku tano kupata miadi ya kumuona daktarin karibu na nyumbani kwake. Aliomba kufanyiwa vipim mwishoni mwa Juma ikiwa ni wiki moja baada ya dalili za mwanzo kujitokeza- uchovu, kuishiwa pumzi, maumivu ya kichwa na maumivu ya koo. Kituo cha afya kilimjulisha kuwa majibu yake yangechelewa.

Maambukizi yanayovunja rekodi

Kwa mujibu wa uchambuzi wa shirika la habari la AP Shughuli za upimaji wa virusi vya corona zimeongezeka kote nchini humo na kufikia wastani wa vipimo 640,000 kwa siku, kutoka vipimo 518,000 kwa siku, wiki mbili zilizopita.

Idadi ya maambukizi mapya kwa siku inazidi 50,000 na kuvunja rekodi kwa kila namna. Upimaji zaidi unasababisha kugunduliwa kwa visa vingi zaidi.

Coronavirus USA Seattle Teststation Drive-Through
Muuguzi Tina Nguyen akiendesha kipimo cha corona kwenye kituo cha upimaji mjini Seattle, Washington, Machi 26,2020.Picha: Reuters/L. Wasson

Lakini kiashiria cha kushtusha ni kwamba asilimia ya vipimo vinavyoonesha idadi ya walioathiriwa inaongezeka karibu nchi nzima, na kufikia takribani asilimia 27% kwa Arizona,19% Florida na asilimia 17% ktika jimbo la South Carolina.

Hata hivyo Mkurugenzi wa Taasisi ya chou kikuu cha Havard ya Global Health Dr Ashish Jha, anasema anashangazwa kuwa miezi sita baada ya janga hii la COVID -19 bado Marekani inashindwa kufanya namna ya kutoa vipimo kwa Wamarekani katika kipindi hiki ambacho wanavihitaji.

Wataalamu wa afya wanaonya kuwa, kupima pekee bila kuwa na utaratibu wa kufuatilia muingiliano wa watu na kucuhukua hatua za kuwaweka karantini hakuwezi kudhibiti kusambaa kwa janga hili.

Lakini wanasema kuchelewesha upimaji kunaweza kusababisha maambukizi zaidi kwa kuwaacha watu njiapanda wasijue kama wanahitaji kujitenga ama la.

Chanzo: Mashirika