1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Katumbi ataka kuungana na Bemba uchaguzi DRC

Sekione Kitojo
26 Juni 2018

Kiongozi wa upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Moise Katumbi, anasema anapendelea muungano ambao unaweza kumjumuisha kiongozi mwingine wa upinzani, Jean-Pierre Bemba.

https://p.dw.com/p/30JYF
Ruanda Kigali - Moise Katumbi Chapwe bei der Mo Ibrahim Award
Picha: DW/E. Topona

Bemba, ambaye anatarajiwa kurejea nchini mwake hivi karibuni, baada ya hukumu dhidi yake katika uhalifu wa kivita kufutwa kutokana na kukata rufaa.

Katumbi, Bemba na Felix Tshisekedi, kiongozi wa chama kikubwa cha upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ni wagombea wakuu,wa  upinzani ambao wanaweza kugombea katika uchaguzi wa rais mwezi Desemba mwaka huu kumchagua mrithi wa rais wa sasa, Joseph Kabila.

Bemba, kiongozi wa zamani  wa waasi  mbaye ni maaruf  na makamu wa rais  aliondoka nchini Congo mwaka 2007, na ametumikia kifungo cha miaka 10 jela mjini The  Hague. Lakini anatarajiwa kurejea nyumbani mwezi Julai na anaweza kushiriki katika uchaguzi.