1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa ziarani mjini New.Delhi

28 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFIb

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Kofi Annan ameitolea mwito India itie saini mkataba wa kusitisha majaribio ya silaha za kinuklea.Akiwa ziarani mjini New-Delhi,katibu mkuu wa Umoja wa mataifa kofi Annan amesema anataraji India itatie saini pia mkataba wa kutosambaza silaha za kinuklea.Serikali ya India inapinga moja kwa moja kuidhinisha mkataba huo wa kutosambaza silaha za kinuklea.Wakati huo huo katibu mkuu wa Umoja wa mataifa amezitolea mwito nchi zanachama wa umoja wa mataifa zifikie maridhiano hadi ifikapo mwezi september ujao kuhusu namna ya kuifanyia marekbisho jumuia hiyo ya kimataifa na namna pia ya kupanua baraza la usalama.