1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mzozo wa corona unakaribia kuwa mzozo wa haki za binadamu

23 Aprili 2020

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema janga la virusi vya corona ni mzozo wa kibinadamu ambao unageuka kwa kasi kuwa mzozo wa haki za binadamu.

https://p.dw.com/p/3bJBA
Coronavirus - UN-Generalsekretär Guterres
Picha: Imago/L. Rampelotto

Katibu Mkuu huyo amesema katika ujumbe alioutoa kwa njia ya vidio leo, kwamba kuna ubaguzi katika utoaji wa huduma za umma kukabiliana na ugonjwa wa covid-19, na kuzungumzia pia ukosefu wa usawa wa kimuundo ambao unazuwia upatikanaji wa huduma hizo.

Guterres amesema janga la corona limesababisha pia athari zisizolingana kwa baadhi ya jamii, kuongezeka kwa matamshi ya chuki, kulengwa kwa makundi ya walio hatarini, na kusababisha hatari ya matumizi ya nguvu iliyopitiliza kwa upande wa idara za usalama, hali inayoodhofisha hatua za kiafya.