1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa anatazamiwa kwenda Sudan na Darfour wiki hii

24 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFAh

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Kofi Annan atakwenda Khartoum ijumaa ijayo kwa mazungumzo pamoja na viongozi wa serikali ya Sudan.Katibu mkuu Kofi Annan amepangiwa pia kuzungumza na wawakilishi wa Umoja wa Afrika na umoja wa mataifa kabla ya kwenda Rumbeke kwa mazungumzo pamoja na kiongozi wa waasi wa zamani John Garang.Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa kofi Annan atatokea Addis Ababa ambako alkhamisi ijayo atasimamia pamoja na mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Alpha Oumar Konare,mkutano wa wafadhili kuunga mkono juhudi za kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika katika jimbo la Darfour.Mwezi uliopita Umoja wa Afrika ulielezea azma ya kuzidisha mara tatu idadi ya vikosi vya kulinda amani katika jimbo la mizozo la Darfour hadi ifikapo mwezi september ujao.