1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Karibu nyumba 1,000 zaharibiwa na upepo mkali Afrika Kusini

8 Julai 2024

Takriban nyumba 1,000 zilizopo katika makazi yasiyo rasmi huko Cape Town nchini Afrika Kusini, zimeharibiwa na upepo mkali, na kupelekea watu wapatao 4,000 kuyahama makazi yao.

https://p.dw.com/p/4i1aS
Afrika Kusini
Karibu nyumba 1,000 zaharibiwa na upepo mkali Afrika KusiniPicha: RAJESH JANTILAL/AFP

Hayo yameelezwa na mamlaka za nchi hiyo pamoja na shirika la misaada wakati jiji hilo likijiandaa kwa wiki nzima ya dhoruba kali. Taasisi ya kuratibu majanga huko Cape Town imekuwa katika hali ya tahadhari tangu Alhamisi wiki iliyopita.

Mafuriko Afrika Kusini yasababisha vifo vya watu 22

Mamlaka ya hali ya hewa ya Afrika Kusini imesema kuwa mji wa Cape Town na maeneo ya jirani yanatarajiwa kukumbwa dhoruba angalau hadi siku ya Ijumaa, hali itakayosababisha mvua kubwa, upepo mkali na mafuriko.