1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Karibu nusu ya Ulaya katika hatari ya kukabiliwa na ukame

18 Julai 2022

Watafiti katika Halmashauri Kuu ya Ulaya wametahadharisha leo kwamba karibu nusu ya eneo la Ulaya liko katika hatari ya ukame.

https://p.dw.com/p/4EIlT
Spanien Miranda de Arga | verbrannte Landschaft nach Waldbränden
Picha: Alvaro Barrientos/AP/picture alliance

Tahadhari hii imekuja wakati ambapo eneo la kusini magharibi mwa Ulaya linakabiliwa na joto kali mno.

Katika ripoti yake ya mwezi Julai, Kituo cha pamoja cha Utafiti cha Halmashauri Kuu ya Ulaya kimesema asilimia 46 ya Ulaya iko katika kiwango cha tahadhari ya ukame, huku asilimia 11 ikiwa katika kiwango cha hatari ambapo mazao yakiwa yanaathirika kutokana na ukosefu wa maji.

Umoja wa Ulaya unasema Italia ndio imeathirika vibaya zaidi na huko Uhispania nako maji katika hifadhi yako asilimia 31 chini ya kiwango cha wastani cha miaka kumi.

Ripoti hiyo inazidi kueleza kwamba nchini Ureno, kiwango cha maji yanayotumika kufua umeme kiko nusu ya wastani ya miaka saba iliyopita.