1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Mafunzo

Karandinga: Chimbuko la Itikadi Kali

10 Novemba 2015

Katika mchezo huu kuhusu Kuenea kwa Itikadi Kali, tunashuhudia bomu linalipuka katika eneo la maduka makubwa huko Kululaland na maafisa vijana wa polisi Jude na Brenda wanakishughulikia kisa hicho.

https://p.dw.com/p/1H3KU
09.2015 Crime Fighters The Radical Journey (Serienmotiv)

Bomu linalipuka katika duka kubwa huko Kululaland na maafisa vijana wa polisi Jude na Brenda wanakishughulikia kisa hicho. Mara wanagundua lilikuwa shambulizi la kujitoa muhanga lililofanywa na msichana. Cha kushtusha zaidi ni utambulisho wake. Mshambuliaji anaitwa Zorah Kassim – amemaliza masomo yake ya chuo kikuu na anatokea kwenye familia tajiri. Kama mtoto wa kike wa mwanasiasa mwenye ushawishi, zipi huenda zilikuwa sababu zake za kufanya shambulizi hilo? Je, alilazimishwa kulifanya? Au alilifanya kwa hiari? Kwa kutumia mbinu tofauti na wakiyahatarisha maisha yao, maafisa Jude na Brenda wanafanya uchunguzi unaofichua taratibu zinazowafanya vijana kujiunga na makundi ya kigaidi. Lakini nia iliyomuongoza Zorah katika safari yake ya kuwa na msimamo mkali wa kidini ni tofauti kabisa. Je kipi kitakachotokea? Na ni nani anahusika na shambulizi hilo la kigaidi? Fuatilia mchezo huu kuanzia mwanzo hadi mwisho wake.