1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Karachi. Kiongozi wa al Qaeda akamatwa nchini Pakistan.

5 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFGa

Majeshi ya usalama ya Pakistan yametangaza kuwa yamemkamata mtu mmoja anayetuhumiwa kuwa ni kiongozi wa Al Qaeda, Abu Faraj al Libbi raia wa Libya. Anatuhumiwa kuwa alipanga kumuua kiongozi wa Pakistan Jenerali Pervez Musharaff miezi 18 iliyopita.

Anaelezwa kuwa mtu wa tatu katika uongozi wa al Qaeda.

Rais wa Marekani George W. Bush amepongeza kukamatwa kwa mtu huyo na kusema kuwa ni ushindi katika vita dhidi ya ugaidi.

Waziri wa mambo ya ndani wa Pakistan amethibitisha kukamatwa kwa mtu huyo katika mkutano na waandishi wa habari katika mji mkuu wa nchi hiyo. Amewaambia waandishi wa habari kuwa al Libbi alikuwa mpangaji wa mambo mbali mbali ya al Qaeda. Watu 17 wameuwawa katika matukio mawili ya kutaka kumuua rais Musharaf Desemba mwaka 2003.