1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaItaly

Scholz kukutana na waziri mkuu wa Italia Giorgia Meloni

8 Juni 2023

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz anafanya ziara leo nchini Italia, kufanya mazungumzo na waziri mkuu wa nchi hiyo Giorgia Meloni.

https://p.dw.com/p/4SKhP
Estland | Bundeskanzler Scholz in Tallinn
Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Hiyo ni ziara yake ya kwanza Italia tangu Meloni, mwanasiasa wa sera kali za mrengo wa kulia alipoingia madarakani Oktoba mwaka jana. Waziri Mkuu Meloni pia alifanya ziara mjini Berlin mwezi Aprili, na wakati huo Kansela Scholz alibainisha nia ya kuendeleza ushirikiano wa karibu na kiongozi huyo mpya, na kuongeza kuwa makubaliano na serikali ya awali yangeendelea kuzingatiwa bila mabadiliko.

Meloni aliishambulia vikali Ujerumani wakati wa kampeini

Wakati wa kampeni akiwa mpinzani, Meloni alikuwa akiishambulia vikali Ujerumani, lakini baada ya kuchukua hatamu za uongozi alipunguza makali ya lugha yake. Mazungumzo kati ya viongozi hao wawili leo hii yanatarajiwa kutuama juu ya uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, na masuala ya Ulaya kama vile sera kuhusu waomba hifadhi.