1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kane asema atahitaji muda wa kuzoea kandanda la Ujerumani

13 Agosti 2023

Nahodha wa timu ya kandanda ya England Harry Kane amesema leo kuwa atahitaji muda ili kulizoea kandanda la Ujerumani. Hii ni baada ya kupoteza mchezo wake wa kwanza katika timu ya Bayern Munich.

https://p.dw.com/p/4V7Jz
Fußball Supercup | FC Bayern München - RB Leipzig | Harry Kane
Picha: Revierfoto/dpa/picture alliance

Kane pia amesema hatokuwa na hofu kama hataanza kufunga mabao. Kane aliingia kutokea benchi katika mechi ya jana usiku ya Kombe la Super Cup la Ujerumani ambayo walipigwa 3 - 0 na Leipzig, baada ya kuthibitishwa kuwa mchezaji wa Bayern mapema jana.

Akizungumza leo wakati akitambulishwa rasmi na klabu hiyo, Kane mwenye umri wa miaka 30, amesema ni wazi kuwa amecheza kandanda maisha yake yote nchini England na katika Ligi ya Premier kwa hiyo atahitaji muda wa kuizoea ligi mpya ya Bundesliga. Bayern waliweka rekodi kwa kumsajili Kane kutoka Tottenham Hotspur kwa zaidi ya euro milioni 120.

Harry Kane alikuwa amebakisha mwaka mmoja pekee kuitumikia Spurs na mmiliki wa klabu hiyo ya London Joe Lewis aliamua kumuuza badala ya baadaye aondoke bure pindi mkataba wake utakapokamilika mwakani.

Kane alipitia chuo cha mafunzo cha soka cha Spurs na ndiye mfungaji bora wa muda wote wa timu hiyo akiwa na mabao 280 katika mechi 435.