1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiGuinea-Bissau

Kampuni ya Uturuki yauzimia mji mkuu wa Guinea Bissau umeme

18 Oktoba 2023

Mji mkuu wa Guinea Bissau umetumbukia gizani usiku wa kuamkia Jumatano baada ya kampuni ya umeme ya Uturuki Karpowership, kuzima umeme unaoingia mji huo kwa sababu ya madeni.

https://p.dw.com/p/4Xf8T
Tangu mwaka 2019, kampuni ya umeme ya Karpowership imekuwa ikikidhi mahitaji ya umeme ya Guine Bissau kwa asilimia 100.
Tangu mwaka 2019, kampuni ya umeme ya Karpowership imekuwa ikikidhi mahitaji ya umeme ya Guine Bissau kwa asilimia 100.Picha: MATIAS BAGLIETTO/REUTERS

Kampuni hiyo imelizimia taifa hilo la Afrika Magharibi umeme kwa sababu ya deni la dola milioni 17.

Waziri husika Suleimane Seidi amesema mipango inawekwa kulipa dola milioni 15 za malimbikizo yanayodaiwa na ameahidi kuwa suala hilo litatatuliwa ndani ya siku 15.

Kampuni ya umeme ya Karpowership imekuwa ikikidhi mahitaji ya umeme ya Guine Bissau kwa asilimia 100, tangu makubaliano yao ya mwaka 2019.

Hiyo ni kulingana na tovuti ya kampuni hiyo ambayo ni kati ya kampuni kubwa ulimwenguni zenye mitambo inayoelea baharini.

Mnamo Septemba, kampuni hiyo ilizima usambazaji umeme katika mji mkuu wa Sierra Leone, Freetown kutokana na deni la takriban dola milioni 40.