1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kampeni ya utoaji wa chanjo ya polio kwa watoto yaanza Gaza

Angela Mdungu
31 Agosti 2024

Kampeni ya kutoa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Polio imeanza katika Ukanda wa Gaza. Afisa wa huduma za Afya Moussa Abed wa wizara ya Afya ya Gaza iliyo chini ya Hamas amesema chanjo zimeanza kutolewa Jumamosi.

https://p.dw.com/p/4k8Vh
GAZA | Kampeni ya chanjo dhidi ya Polio kwa watoto
Watoto wameanza kupatiwa chanjo dhidi ya polio Ukanda wa GazaPicha: Hani Alshaer/Anadolu/picture alliance

Zoeji hilo limeanza japo awali maafisa walitangaza kuwa chanjo hiyo ingeanza rasmi kutolewa Jumapili.

Soma zaidi: Israel kusitisha mapigano Gaza kwa siku 3 kupisha chanjo ya Polio

Shirika la Afya duniani WHO lilitangaza Alhamisi kuwa, Israel imekubali kusitisha mapigano kwa muda ndani ya siku tatu ili kuruhusu utolewaji wa chanjo hizo. Utoaji wa chanjo hizo kwa maelfu ya watoto Kusini na kisha Kaskazini mwa Gaza unafanyika wakati  wizara ya afya ya  ukanda huo ikisema kuwa hadi sasa Wapalestina  40,691 wameuwawa tangu Oktoba 7.